Infinix kuja na kamera ya juu

0
14

Kwa sisi wafuatiliaji wazuri wa mambo ya teknolojia tunafahamu toleo la Infinix S5 pro si hadithi tena kwao ila kwa nchi kama Tanzania bado ni kitendawili kisicho na mteguzi kwani hivi punde kupitia mitandao ya kijamii kuna walio thubutu kuilinganisha Infinix S5pro na simu za makampuni mengine zinazotarajia kutoka mwaka huu kama TECNO Camon 15 na hapo ndipo vuta nikuvute ilipoanzia huku kila mdau akitetea hoja yake;

Nanukuu; hauezi fananisha Infinix s5pro kwa simu ya kampuni yoyote kwa sasa achilia mbali hiyo TECNO camon 15 inayosemekana kuwa na megapixel 48 selfie kamera kama ya Infinix S5pro.

Hivi kwanza mnafahamu kamera ya S5 pro kama ipo juu na ndio simu ya kwanza kwa mwaka huu kuja na ubunifu wa aina yake pasipo kuwa na bei ya kuumiza wateja wake.

Na baada ya kuinadi vyema kamera ya Infinix S5pro yenye megapixel 48 za Selfie Kamera pia aligusia kuhusiana na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu (memory card) akidai kuwa Infinix S5pro kuja na GB 128 ROM na RAM ya GB 6.

Nikiwa kama mwandishi siwezi pinga wala kukubali moja kwa moja ila kwa upande wa kamera na battery simu za Infinix zinaongoza kwenye huo ubora na unaweza jithibitishia kupitia matoleo ya awali kama Infinix S4 iliyoonekana kukimbiza kwenye kamera na Infinix HOT 8 iliyotikisha kwa battery na msemo wake wa ikijaa imejaa, hivyo basi tutegemee mazuri ya Infinix S5pro ipo juu.

Send this to a friend