INFINIX KUMALIZIA MWAKA NA NOTE.

0
37
                                                     

Infinix mbioni kutamba tena na toleo la NOTE na hii ni baada ya toleo la awali la Infinix NOTE 7 vizuri sokoni. kupitia mtandao wao @infinixmobiletz wameashiria kuna ujio wa simu mpya yenye sifa zifuatazo;
• Helio G80 processor
• 64MP Ultra HD 6 kamera
• 5200mAh battery.

Huku ikiwa kampuni haijataja ni toleo gani hilo lakini wadau wa simu za Infinix wamekuwa wakitabiri huwenda toleo hilo jipya ni Infinix NOTE 8 na kutokana na baadhi ya sifa nilizotaja hapo juu. Inasemekana toleo la NOTE ni moja ya toleo lenye ubora kama ilivyo kwa toleo la Infinix ZERO.


Tukiwa bado hatujafahamu sifa nyengine za simu hiyo inayosemekana huenda ni Infinix NOTE 8 lakini tunafahamu Infinix ni kampuni imara yenye kuzalisha simu zenye viwango vya hali ya juu kwa bei ambayo Mtanzania mwenye uchumi wa hali yoyote anaweza kuimudu.


Kwa uchache wa sifa tulizozinyaka inaonekana simu hiyo itakuwa tishia kutokana na aina ya processor Helio G80 kuwa processor yenye kuhimili application zenye ujazo wowote. Processor ya Helio G80 pamoja ya kuhimili application zenye ujazo mkubwa lakini pia inapunguza kasi ya simu kuisha chaji, inazuia simu isipate moto kwa matumizi ya muda mrefu na kuziendesha application kama za games na nyenginezo pasipo kuzembea zembea.


Bado maswali yanabaki kwetu hadi pale tutakapompata Aisha Karupa Afisa wa mahusiano wa kampuni ya Infinix azungumze nasi simu hiyo ni simu gani, sifa nyengine za simu hiyo na bei yake.

Send this to a friend