INFINIX KUTANGAZA RASMI UWEPO WA TOLEO JIPYA – INFINIX HOT 10.

0
38

Tanzania, Dar es Salaam, 10/10/2020-Infinix, kampuni bingwa ya uzalishaji wa simu za mkononi imetangaza rasmi uwepo wa toleo jipya katika matoleo ya HOT.

Infinix HOT 10 iliingia rasmi mwanzoni mwa week hii katika maduka ya simu nchini Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya simu zote zenye thamani ya Sh.300,000 had Sh.350,000. Ni simu iliyotokea kupendwa na vijana zaidi na hii ni kwasababu imebeba sifa zifuatazo kama vile; Processor aina ya MediaTek Helio G70, battery yenye ujazo wa 5200mAh, kamera zenye megapixel 16+2+2+QVGA kwa megapixel 8 selfie, memory yenye GB 64+GB 3RAM, kioo cha nchi 6.78 na teknolojia ya DTS Audio.

Infinix HOT 10 ni simu yenye kuwalenga vijana wa kisasa wenye kupenda kwenda na wakati lakini pia ni simu ya kwanza katika matoleo ya HOT Series kuwa na processor yenye kasi aina ya MediaTek Helio G70 na teknolojia ya MediaTek HyperEngine. MediaTek HyperEngine inakazi nyingi katika uchezaji games na kazi moja wapo ni kubeba na kuendesha games zenye ujazo mkubwa pasipo kuzidiwa mzigo.

Kioo cha Infinix HOT 10 chenye Inch 6.78 humsaidia mtumiaji kueka application zake katika mpangilio mzuri na kuziona katika hali ya ukubwa zaidi. Infinix HOT 10 haina mvuto katika upande wa kioo tu lakini hata umbo lake linawembamba wa mm9, hivyo unaweza kuihifadhi hata katika mfuko wa surual au shirt pasipo kuharibu show ya muonekano wako.

Teknolojia ya AI yenye megapixel 8 za selfie na megapixel 16 zinapiga picha zenye uhalisia pasipo kujali nyakati wala mazingira, kamera hizi mbili zinateknolojia ya AI smart beautification na super night view mode kwajili ya ung’arishaji picha katika nyakati zote.

“Battery ya HOT 10 yenye ujazo wa mAh 5200 inadumu na chaji kwa kipindi cha muda mrefu hata pasipo kuzima data ya simu yako na huku ukiendelea kucheza magemes na kujiburudisha na mziko mzuri unaochunjwa kwa kutumia teknlojia ya DTS Audio” alisema Afisa wa Mahusiano wa Kampuni ya simu Infinix Mobility, Aisha Karupa.

Infinix HOT 10 inapatikana katika rangi mbalimbali kwenye maduka yote ya simu nchini Tanzania na ili kufahamu zaidi kuhusiana na bidhaa za Infinix tafadhali tembelea @infinixmobiletz .

Send this to a friend