Infinix Note 7 simu yenye teknolojia kali kuzidi zote kwa mwaka 2020

0
109

Dar es Salaam, Tanzania-5/5/2020: Kupitia kurasa zao pendwa za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz kampuni ya simu ya Infinix imezindua rasmi sifa za simu mpya aina ya Infinix NOTE 7 au unaweza iita BIGIMAKINI. Infinix NOTE 7 ni simu yenye sifa lukuki zenye kuvutia kuanzia umbo lake kubwa lenye upana wa kioo cha nchi 6.95 na megapixel 48 kamera pamoja na kasi ya processor aina ya MediaTek Helio G70.                                                             

Processor ya G70 inakasi kubwa yenye kuwezesha matumizi mbali mbali ya kiofisi na yasiyoyakiofisi kama vile games zinazoitaji speed kubwa bila kuchoka na miongoni mwa sifa nyengine za Infinix NOTE 7 ni uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu pasipo uhitaji wa kuichaji kwa muda mwingi kutokana na uwezo mkubwa wa battery yenye mAh 5000 na teknolojia ya fast charge. Sifa yingine zenye kuifanya Infinix NOTE 7 kuwa simu yako bora kwa mwaka huu wa 2020 ni ukubwa wa memory ya GB 128ROM + 6RAM.                                                          

Kwa mwaka huu wa 2020 Infinix NOTE 7 ndio simu kubwa zaidi kutolewa na kampuni hii ya Infinix lakini kutoka na ugonjwa ambao unaikumba dunia nzima kwa ujumla Infinix imelegeza bei kwa wateja wake na simu hii itapatikana madukani kwao Infinix Smart Hub Mlimani City na Smart Hub Kariakoo kwa bei isiyozidi 480,000 za kitanzania.                                              

Vile vile Infinix inakupa nafasi ya kujishindia Infinix NOTE 7 nyingine mpya kwa mteja yoyote wa Infinix NOTE 7 atakayepiga picha box la simu baada ya kununua na kupost kwenye mtandao  wa kijamii na kuambatanisha na #tag ya #BIGIMAKINI, na zawadi nyengine kama vile magic cup, Notebooks, Speaker hutolewa papo hapo.

Send this to a friend