Isemavyo Katiba ya Tanzania kiti cha Spika wa Bunge kinapokuwa wazi

0
52

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo Januari 6, 2022 kwa hiari yake mwenyewe kwa kulinda maslahi ya Taifa, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (84) ibara ndogo ya 8 inaeleza kwamba, pindi kiti cha spika itakapokuwa wazi, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha Spika kitakuwa ki wazi.

Hii inamaanisha kwamba, ili shunguli za bunge linalotarajiwa kuanza Februari 1, 2022 ziweze kuendelea, ni lazima kwanza limchague Spika.

Wasifu wa maisha ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Kwa mujibu wa katiba, (84)(1), spika atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

Ibara ya 86(3) inafafanua zaidi kuwa uchaguzi wa Spika, na vile vile uchaguzi wa Naibu wa Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

Katiba inaeleza kuwa, spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-

(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge; au

(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa Spika; au

(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa, lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya Katiba hii; au

Isome hapa barua ya kujiuzulu ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ajiuzulu

(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote; au

(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo (5) ya ibara hii; au

(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii; au

(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na Bunge;

(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

Send this to a friend