Ishara 5 anazoonesha mtu ambaye anataka kujiua

0
59

Baadhi ya visababishi vinavyoweza kusababisha mawazo ya kujiua kwa mtu binafsi vinaweza kutofautiana kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali yakiwemo kitaaluma au ya kifedha, unyanyasaji, hali ya kutengwa, maumivu ya kudumu na masuala mengine ya kibinafsi.

Kujiua kunaweza pia kuwa matokeo ya baadaye ya matatizo makubwa ya akili kama vile unyogovu, wasiwasi, mfadhaiko, ugonjwa wa bipolar na kadhalika.

Dkt. Kedar Tilwe, Mtaalamu na mshauri wa Saikolojia kutoka hospitali ya Fortis huko Mulund na Vashi, anatoa ishara tano za onyo za tabia ya kujiua ambazo hazipaswi kupuuzwa:

1. Historia ya awali ya kujaribu kujidhuru

Ikiwa una historia ya majaribio ya kutaka kujidhuru basi umakini unahitajika zaidi, pengine kukawa na uwezekano wa tukio hilo kujirudia tena .

2. Kuongezeka kwa unywaji wa pombe

Unywaji wa pombe husababisha uamuzi usiofaa na kupunguza kizuizi, ambayo inaweza kusababisha kupata msukumo wa kutenda jambo baya. Ikiwa kuna ongezeko la matumizi yoyote ya dawa za kulevya, ikiwa ni pamoja na bangi, pombe na tumbaku inaweza kuwa ishara ya hatari.

3. Tabia ya kujidhuru

Ikiwa una michubuko na mikwaruzo yoyote katika mwili wako isiyoelezeka au isiyotarajiwa ambayo hujisababishia mwenyewe unapokuwa na hasira, hiyo ni ishara ya hatari ambayo unapaswa kuwa makini na kutoipuuzia.

4. Mabadiliko yasiyo ya kawaida ya tabia

Mabadiliko ya ghafla ya tabia kama vile kujiondoa katika jamii, kupunguza mawasiliano na wakati mwingine hata maombi ya mara kwa mara ya kuomba msamaha kutokana na hisia zinazoonekana kuwa na hatia au makosa, yanapaswa kutumika kama ishara ya hatari isiyopaswa kupuuziwa.

5. Kutishia au kuzungumza kuhusu kujiua

Dokezo lolote, ishara au historia inayoonesha uwezekano wa nia ya kujidhuru ni alama nyekundu inayotakiwa kushughulikiwa. Mtu anayepitia mambo haya anapaswa kuzungumza na mtaalam wa saikolojia kwa upole pasipo kumhukumu.

Send this to a friend