Ishara 5 zinazoonesha unaweza kuwa rafiki na ex wako

0
63

Kulingana na mtaalamu wa masuala ya ndoa na familia nchini Marekani, Weena Cullins inawezekana kabisa kuwa marafiki na mpenzi wako wa zamani.

Ikiwa wewe na mwenza wako wa zamani mtatambua kuwa nyinyi ni washirika wazuri wa kibiashara au jambo lolote, na wote mnaweza kuweka mipaka yenye nguvu kati yenu, kuwa marafiki kunaweza kufanikiwa, amesema.

Ameongeza kuwa ikiwa wewe na mwenza wako wa zamani mna watoto pamoja, kuwa marafiki itatengeneza mazingira rahisi kwa watoto wenu.

Wakati gani unaweza kuwa rafiki na ex wako?

• Ikiwa nyote wawili mmekubali kwamba uhusiano umekwisha na kuelewa kwa nini umekwisha.

• Unahisi kuwa huna hisia nae tena, na mpenzi wako wa zamani hana hisia za kimapenzi na wewe.

• Wewe na mpenzi wako wa zamani mnaweza kutumia muda pamoja bila kuhisi hasira, wasiwasi, maumivu au wivu.

• Nyote wawili mnahisi kufurahia kabisa kuwa kwenye mahusiano na watu wengine.

• Mna watoto pamoja au shughuli zenu zinawakutanisha pamoja kwa namna fulani.

Je! Unaweza kuwa rafiki na ex ambaye bado unampenda?

Ikiwa mapenzi uliyo nayo kwa mpenzi wako wa zamani bado ni mazito, kuwa kwenye urafiki naye kunaweza kufanya iwe vigumu zaidi kwako kuuacha uhusiano huo na kusonga mbele.

Send this to a friend