Ishara 7 zinazoonesha kuwa mpenzi wako wa kike ana-cheat

0
63

▶️ Kila mtu anapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi anatamani uwe wa watu wawili tu, lakini kuna wakati mmoja hukosa uaminifu na kuanza kutoka nje ya uhusiano kwa siri.

▶️ Licha ya uwepo wa usiri, ishara kama kupunguza mawasiliano, kuficha simu, kutaka kuwa mwenyewe vinadokeza kwamba kuna jambo haliko sawa, ni wewe kufuatilia.

Hakuna mtu anayetaka kuamini kuwa mpenzi wake anamdanganya kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine. Ikiwa unahisi kuwa mpenzi wako sio mkweli, fuatilia ishara hizi zitakazokuongoza kupata majibu ya maswali yako.

1. Anajitahidi kukuweka mbali na simu yake
Ikiwa mpenzi wako anaficha simu yake mara kwa mara ili usiione au amebadilisha nywila ili usiipate, hizi zinaweza kuwa ishara kwamba anakudanganya. Anapojitahidi kuhakikisha kuwa huoni ni nani anatuma ujumbe, inaweza kuwa hataki ujue kuwa kuna mtu mwingine zaidi yako.

2. Anapunguza mawasiliano
Unakumbuka siku za mwanzo za uhusiano wenu alipokuwa akikuambia chochote na kila kitu kuhusu maisha yake? Ikiwa ghafla hataki kuzungumza juu ya mambo yake au anaepuka maswali kuhusu mahali alipokuwa au alikuwa na nani, inawezekana kwamba tayari anakudanganya au amepoteza hamu katika uhusiano huo.

3. Anatamani kujua ratiba yako
Mbali na kuwa msiri zaidi kuhusu mahali aliko, wapenzi wakike wanaodanganya mara nyingi huwa na hamu ya kutaka kujua waliko wapenzi wao ili kujua ni lini hasa utakuwa mbali ili waendelee na mambo yao kwa usalama zaidi.

4. Anatafuta makosa
Wakati mwingine wanawake huwa na tabia ya kuanza kuwalaumu wapenzi wao zaidi licha ya kuwa wao ndio wanakosa uaminifu. Sababu moja ni kwamba wanatafuta makosa kwa wapenzi wao ili waweze kuhalalisha ‘cheating’ yao. Anaweza pia kuwa anaona mabaya zaidi kwako kwa kukulinganisha na mpenzi wake mpya, wakati mwingine inaweza kuwa njia ya yeye kukufanya uachane naye.

5. Anakuwa kimya
Ikiwa mpenzi wako anakuwa kimya ghafla na kutojihusisha na mtu hata akiwa kwenye sherehe au na marafiki zake, kuna uwezekano kwamba anafikiria kuhusu mtu mwingine. Mawazo ya kina ni ishara nzuri kwamba yeye hajishughulishi kiakili au kihemko na uhusiano wako kama alivyokuwa hapo awali.

Mbinu 5 za kuanzisha mazungumzo na msichana uliyekutana naye mara ya kwanza

6. Rafiki mpya asiye na jina
Ikiwa mpenzi wako ana rafiki mpya ambaye humtaja mara kwa mara lakini bado hana jina au hataji ni aina gani ya shughuli wanazofanya pamoja, inawezekana kwamba yeye ni zaidi ya marafiki tu. Mojawapo ya njia unazoweza kujua zaidi kuhusu uhusiano wao ni kumwalika rafiki yake mpya, ikiwa atakataa au kutoa visingizio, anaweza kuwa anakulaghai.

7. Kumtilia shaka
Ikiwa unahisi kutiwa shaka zaidi na shughuli zake wakati hayuko na wewe hadi kufikia hatua ambayo unatamani kuacha kazi zako ili tu kumfuata na kuhakikisha kile anachofanya kila dakika, basi ni ishara ya uhakika kwamba kuna kitu kibaya kwenye huo uhusiano. Huenda kuna mabadiliko ambayo yamekufanya kuwa na shaka naye, au kitu ambacho alisema na hakikukaa sawa ambacho kilianzisha shaka ndani yako.

Mwisho wa siku, jambo bora unaweza kufanya ni kumuuliza tu. Kuwa tayari kwa majibu yake kwa njia yoyote ile, na kumbuka kuwa mara nyingi kudanganya sio jambo ambalo alifanya ili kukuumiza kwa makusudi. Kawaida ni dalili ya uhusiano usiofaa ambao labda ulikuwa unaelekea kuvunjika mapema au baadaye, kwa hivyo hakuna kati yenu anayepaswa kulaumiwa.

Send this to a friend