Ishara 8 zinazoashiria uko katika uhusiano na mtu anayeaminika

0
55

Kuaminiana ni moja ya mambo muhimu katika uhusiano. Hutuwezesha kujisikia salama, hutoa ulinzi na kutusaidia kujenga na kuimarisha mahusiano.

Ikiwa hamwamini mpenzi wako, inaweza kukufanya utilie shaka uhusiano huo na kufikiria mambo mengi mabaya kuhusu yeye.

Hizi ni baadhi ya ishara zinazoonesha kwamba uko kwenye uhusiano na mtu unayeweza kumwamini na kumtegemea.

Hutimiza ahadi zake
Jambo moja ambalo mtu mwaminifu hufanya kila wakati ni kutimiza ahadi zake. Ni rahisi kutoa ahadi, lakini ni vigumu kuitimiza. Ikiwa mpenzi wako hutimiza neno lake hata katika hali ngumu, una uhakika kwamba umepata mtu unayeweza kumtegemea.

Muwazi
Mtu ambaye ni mwaminifu anajua kuwa hakuna kitu kibaya zaidi kama kutoeleweka. Mpenzi wako anapokuwa muwazi hasa linapokuja suala nyeti, inamaanisha kuwa anaweza kuaminiwa. Hii ni ishara kuwa anakuthamini vya kutosha kutaka kujadili jambo ambalo linaweza kuathiri jinsi unavyomchukulia.

Haendekezi kiburi chake
Unaweza kumwamini mpenzi wako ikiwa yuko tayari kufanyia kazi udhaifu wake, si kwa ajili yako tu bali pia kwa ajili yake mwenyewe.

Mambo 4 ya kuzingatia kabla ya kununua pete ya uchumba

Anajali
Ikiwa anakupa sababu nyingi mara kwa mara hasa pindi unapokuwa katika changamoto fulani anaweza asiwe mtu wa kumwani au kumtegemea. Mtu anayeaminika, utamjua kutokana na jinsi anavyoonesha kujali.

Huvutiwa na wewe zaidi kuliko kile unachoweza kumpa
Ikiwa kipaumbele chake ni wewe zaidi kuliko kile ulichonacho ama unachompa, basi anaweza kuaminika. Upendo utokao ndani huambatana na uaminifu pia.

Anaheshimu wengine
Kuwaheshimu watu wengine pia ni ishara nzuri kuwa unaweza kumwamini. Ikiwa uko katika uhusiano na mtu anayeaminika, sifa yake hiyo nzuri pia itaenea kwa watu wengine.

Anajitoa kwako
Ikiwa unataka kujua kama mpenzi wako anaaminika au la, utaona jinsi anavyojitoa kwako. Kila muda atakuwa tayari kutoa msaada bila kujali itachukua muda gani.

Anatunza siri zako
Mpenzi anayeweza kuwaeleza marafiki zake mambo ya ndani kuhusu wewe, kamwe hawezi kuaminika.

Send this to a friend