Isome hapa mikataba sita iliyosainiwa kati ya Tanzania na Ufaransa

0
24

Serikali za Tanzania na Ufaransa zimetia saini jumla ya mikataba sita ya makubaliano kwa nia ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Mikataba na makubaliano hayo ni;

  • Framework Agreement between the Government of the French Republic and the Government of the United Republic of Tanzania Concerning the Financing, Development and Implementation of Priority Strategic Projects in the United Republic of Tanzania

Mkataba wa Awali kati ya Serikali ya Jamhuri ya Ufaransa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati nchini 

  • Credit Facility Agreement, amounting to Euro 178,000,000.00 to support the Construction of Phase 5 of the Bus Rapid Transit (BRT) network in Dar es Salaam Project

Mkataba wa Mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 178 (kati ya Serikali ya Jamhuri ya Ufaransa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka awamu ya tano jijini Dar es Salaam 

  • Credit Facility Agreement, amounting to Euro 80,000,000.00 to enhance Tanzania Agricultural Development Bank’s financial and Institutional capacities to achieve its objective of providing short, medium- and long-term financing to Agricultural sector;

Mkataba wa Mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 80 (kati ya Serikali ya Jamhuri ya Ufaransa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kwa ajili ya kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ili kufikia malengo ya kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta ya kilimo 

  • Grant Agreement, amounting to Euro 1,000,000.00 also to enhance Tanzania Agricultural Development Bank’s financial and institutional capacities to achieve its objective of providing short, medium- and long-term financing to Agricultural sector

Mkataba wa msaada wenye thamani ya Euro milioni moja (1) (kati ya Serikali ya Jamhuri ya Ufaransa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kwa ajili ya kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ili kufikia malengo ya kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta ya kilimo

  • Declaration of Intent between the President of the French Republic and the President of the United Republic of Tanzania Relating to Cooperation in the Area of the Blue Economy and Maritime Safety

Tamko la nia kati ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ushirikiano katika eneo la uchumi wa Buluu na usalama wa bahari

  • Declaration of Intent between the President of the French Republic and the President of the United Republic of Tanzania Regarding Cooperation in Transport Infrastructures and Sustainable Development in the United Republic of Tanzania 

Tamko la nia kati ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ushirikiano katika miundombinu ya usafiri maendeleo endelevu nchini 

  • Memorandum of Understanding between Tanzania Airports Authority and Bouygues Batiment International for Conducting of Feasibility Study for the Rehabilitation of Terminal II at Julius Nyerere International Airport

Hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na Kampuni ya Bouygues Batiment International kwa ajili ya kufanya Upembuzi Yakinifu kuhusu ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Jengo la pili la Abiria – Terminal II).

Send this to a friend