Israel: Wanafunzi wawili wa Kitanzania bado hawajulikani walipo

0
33

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua amesema bado hawajapata taarifa juu ya wapi walipo wanafunzi wawili kutoka Tanzania ambao wapo nchini humo kwa ajili ya masomo, baada ya kupoteza mawasiliano nao toka nchi hiyo iliposhambuliwa na kundi la Hamas mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza katika mahojiano na BBC amesema “Sisi kama ubalozi tumetumia kila namna tunavyoweza kutafuta ukweli wa hawa ndugu zetu. Wako wapi au nini kimetokea, hivyo tutakapopata taarifa sahihi tutazitoa.“

Balozi Kallua aliimbia BBC kuwa wanaendelea kufuatilia hali ilivyo katika maeneo mbalimbali na kuhakikisha watanzania wote wako salama ikiwemo kubaini walipo raia hao wawili.

“Hatuwezi kutoa taarifa za kukisia na tunaendelea kufuatilia kwa mamlaka za Israel ili kupata taarifa sahihi [..] sisi tuko hapa ‘on the ground‘ tunafuatilia watanzania wote waliopo hapa, kuhakikisha usalama wao,“ ameeleza.

Chanzo: BBC Swahili

 

 

Send this to a friend