
Mkuu wa Jeshi la Iran, na afisa wa kijeshi mwenye cheo cha juu zaidi nchini humo, Mohammad Bagheri ameuawa katika mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Israel mapema leo.
Mashambulio hayo pia yamemuua Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC), Hossein Salami, Naibu Kamanda wa Jeshi la Iran, Gholamali Rashid na wanasayansi kadhaa wa nyuklia.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa oparesheni hiyo iliyopewa jina la ‘Operation Rising Lion’ itadumu kwa siku nyingi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa Marekani haikuhusika wala kusaidia mashambulizi hayo kwa njia yoyote.