Itazame video ya kwanza kuwekwa YouTube miaka 15 iliyopita

0
37

Me at the zoo ndio jina la video ya kwanza kabisa kuwekwa katika mtandao wa YouTube. Video hii iliwekwa Aprili 23, 2005 saa 20:31:52, na aliyeiweka ni Jawed Karim ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mtandao huo.

Video hiyo ilirekodiwa na rafiki wa Karim, Yakov Lapitsky ambaye walikuwa wakisoma pamoja shule.

Video yenyewe yenye urefu wa sekunde 18 ilichukuliwa (shot) katika Bustani ya Wanyama ya San Diego ambayo inamuonesha Karim akiwa mbele ya tembo akielezea mikonge yao.

Akauti ya Karim iliyopewa jina “Jawed” ambayo ndimo video hiyo ilipowekwa, ilitengenezwa siku hiyo hiyo.

Itazame video hiyo hapa chini;

Mtandao huo umeleta mapinduzi makubwa katika kushirikishana video ambapo zaidi ya watu bilioni 1.3 wanatumia mtandao huo, huku video zenye urefu za zaidi ya dakika 300 huwekwa kwenye mtandao huo kila dakika moja.

Send this to a friend