Jafo aagiza kukamatwa mfanyabiashara aliyetelekeza makontena bandarini

0
51

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo ameagiza kukamatwa kwa Kaissy, Mkurugenzi wa Kampuni ya Seif for Tobacco Trading Co. Ltd aliyeingiza nchini makontena zaidi ya mia tano (500) yenye malighafi ya Molasesi iliyoharibika na kuyatelekeza katika Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Jafo ameagiza hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia makontena hayo yakiwa yametelekezwa bandarini hapo na mengine kutawanywa katika baadhi ya bandari kavu jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu katika kusimamia mazingira hatuna mzaha, afya za binadamu na mimea ni dhamana yetu, sitaruhusu afya za Watanzania kuwekwa rehani,” Jafo amesisitiza.

Imebainika kuwa mfanyabiashara huyo aliingia nchini kwa hati ya utembezi (tourist) na baadaye kupatiwa kibali cha uwekezaji kupitia Export Processing Zone (EPZA) kilichomruhusu kuwekeza katika uzalishaji wa shisha kibali ambacho kilifutwa baada ya kugundulika kuwa kuna udanganyifu mkubwa kuhusu uwekezaji wake.

Send this to a friend