Jafo ashauri majeshi na shule kuachana na kuni na mkaa

0
33

Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amehimiza shule zote za sekondari (Binafisi naza Serikali) nchini kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kama nishati ya kupikia, na badala yake wajikite katika matumizi ya nishati mbadala.

Waziri Jafo amesema matumizi ya kuni na mkaa yanachochea uharibifu wa mazingira hali inayosababisha misitu kuisha na kuzitaka taasisi za majeshi, Shule za Sekondari kote nchini kujikita katika matumizi ya nishati mbadala.

TRA kutaifisha magari yenye namba zisizotambulika

Meneja masoko na uhusiano ya umma kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Geofrey Meena amesema shirika hilo limezindua matumizi ya mkaa mbadala ili watu wasikate miti kwa lengo la kutunza mazingira.

Waziri Jafo amewataka STAMICO kuongeza kwa wingi uzalishaji wa mkaa mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa Watanzania na taasisi mbalimbali hapa nchini.

Send this to a friend