Jaji kesi ya Mbowe na wenzake ajitoa

0
10

Jaji Elinaza Luvanda amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu, baada ya watuhumiwa hao kuieleza Mahakama Kuu kwamba hawana imani na jaji huyo katika kutenda haki kwenye kesi inayowakabili.

Uamuzi huo umekuja wakati mahakama huyo Divisheni ya Makosa ya Rushwa Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kutoa uamuzi wa katika pingamizi la awali lililowekwa na washtakiwa hao wakidai hati ya mashitaka ina kasoro za kisheria zisizorekebishika, na hivyo kutaka mashitaka kutupiliwa mbali.

Kwa upande jamhuri ilipinga madai hayo na kusema kuwa hati hiyo haina kasoro na kwamba imekidhi masharti ya kisheria.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohamed Abdillahi Ling’wenya, makomandoo waliofukuzwa jeshini kutokana na sababu mbalimbali.

Send this to a friend