Jaji Mkuu: Hakuna mtu anayeweza kumlazimisha hakimu namna ya kuamua kesi

0
61

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumlazimisha hakimu kuamua kesi kwa njia fulani, kwani miiko ya kazi hiyo hairuhusu.

Prof. Juma amesema hayo wakati wa kuwapisha mahakimu wapya 29 wa Mahakama za Mwanzo, hafla iliyofanyika leo mkoani Dar es Salaam.

“Hakuna mtu yeyote anayetakiwa kukuingilia. Hata Jaji Mkuu hawezi kukupigia simu na kukuambia kwamba hiyo kesi iliyoko mbele yako iamue hivi. Ukjiona anakupigia simu ya aina hiyo, moja kwa moja mpeleke mbele ya tume ya utumishi wa mahamaka kwa sababu hiyo ndiyo miiko,” amesisitiza Prof. Juma.

Aidha, amewataka watuhumishi hao wapya kuzungumza na ndugu zao pia, ili wajue miiko ya kazi yao kwamba wasitarajie kwa vile ndugu yao ni hakimu, basi watapata upendeleo kwenye masuala ya kisheria.

“Leo jioni wananchi wengine watakuwa wameanza kujipendekeza pendekeza kwenu, mjihadhari sana,” ameonya.

Ametumia jukwaa hilo kuwatahadhari juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii, mathalani makundi na WhatsApp na kuwawataka kutokutoa taarifa za mahakama ambazo hawapaswi kuzitoa.