Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema jalada la kesi ya tukio la ukatili inayomkabili mbunge wa Babati, Pauline Gekul limefikishwa kwenye ofisa ya mashtaka ya Mkoa (DPP) ili kufikishwa mahakamani.
Katabazi amesema bado wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa watatu huku akibainisha kuwa kila mtu aliyetajwa kuhusiana na tukio hilo ataitwa na kufanyiwa mahojiano.
“Hadi sasa tunawashikilia watuhumiwa watatu ambao hatuwezi kutaja majina yao kwa sababu ya upelelezi ambao ukikamilika tutawafikisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa,” amesema.
Katika hatua hnyingine, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Manyara kimesema kinamsubiri mbunge huyo amalizane na mahakama juu ya mashtaka yanayomkabili ili waweze kumhoji.
Mbunge Gekul anakabiliwa na tuhuma za kumfanyia ukatili kijana Hashimu Ally kwa kuamuru vijana wake kumuingia chupa sehemu ya haja kubwa kama adhabu kwa kile alichoeleza (Gekul) kuwa alitumwa kimkakati katika biashara yake.