Jaribio la kupindua serikali ya Sudan ladhibitiwa

0
54

Serikali ya Sudan imeripoti kuwa kumetokea jaribio la kuipindua serikali kijeshi lakini limedhibitiwa na sasa juhudi za kurejesha hali ya amani linaendelea.

Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limesema kuwa jaribio hilo liliambatana na mpango wa kutwaa jengo ambalo linatumiwa pia na Shirika la Utangazaji la Sudan.

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo, amesema mahojiano na watuhumiwa wa jaribio hilo yataanza muda mfupi ujao.

Send this to a friend