![](https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/jay-z-Diddy-122624-31a2592825304b8e8242fbc5bae0092f-905x613.jpg)
Mwanamke anayejulikana kwa jina la Jane Doe mbaye alidai Sean ‘Diddy’ Combs na Jay-Z walimfanyia unyanyasaji wa kingono miaka 25 iliyopita, ameondoa kesi yake dhidi yao kwa hiari.
Hati hiyo iliwasilishwa na wakili Tony Buzbee, anayewakilisha waathiriwa kadhaa katika kesi zinazohusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Combs.
“Kwa kusimama kidete dhidi ya madai ya uongo na ya kutisha, Jay amefanya jambo ambalo ni wachache wanaweza kufanya hivyo, alikabiliana nayo, hakukubali makubaliano yoyote, hakulipa hata senti moja, ameshinda na kusafisha jina lake,” amesema wakili wa Jay Z, Alex Spiro katika taarifa yake.
Doe awali aliwasilisha kesi dhidi ya Combs mwezi Oktoba na baadaye kuongeza jina la Jay-Z mwezi Desemba, ambapo alidai alidungwa dawa za kulevya na kubakwa baada ya tafrija ya Tuzo za Muziki za MTV mwaka 2000, akiwa na umri wa miaka 13.