Je! Nini maana ya Bibi Harusi kuvaa gauni jeupe na kujifunika kwa Shela?

0
85

Imekuwa ikichukuliwa kama desturi kwa bibi hausi kuvaa vazi la harusi katika siku yake maalum ya kufunga ndoa. Licha ya mavazi haya kuvaliwa kwenye harusi nyingi inaelezwa kuwa mavazi haya hutafsiri maana kadhaa.

Leo nimekuandalia maana ya kila anachokivaa bibi harusi siku ya ndoa.

Gauni jeupe: Kwa mujibu wa imani ya Kikristo, vazi jeupe ni alama ya utakatifu. Ni kusimama mbele za Mungu na mashahidi ya kuwa wewe umeishi maisha matakatifu. Kwa maneno mengine inamaanisha kuwa maisha yako yameoshwa na kutakaswa kwa damu Yesu.

Shela: Maana halisi ya shela ni ushahidi  mbele za Mungu na mashahidi wote ya kuwa binti huyo hajawahi kufunuliwa utupu wake na mwanaume mwingine yeyote.

Bibi harusi anapoingia kanisani kufunga ndoa hufunika uso kwa shela yake, kisha bwana harusi ndiye anayemfunua. Hii ina maana kuwa bwana harusi ndiye mwanaume wa kwanza aliyeruhusiwa na Mungu kufunua utupu wa binti huyo.

Mambo 5 unayofanya kila siku yanayopunguza muda wako wa kuishi

Taji la bibi harusi: Kwa kawaida mtu huwa hajivalishi taji bali huvalishwa baada ya kupata ushindi fulani na kuonesha kuwa ameshindana vema. Kwa upande wa bibi harusi, ni ishara ya tangazo kuwa pamoja na majaribu, vishawishi na tamaa za mwili, amevipiga vita vizuri vya kiimani, na kwamba anatangaza kuwa kwa neema ya Mungu amevishinda.

Je! Ulikuwa unafahamu haya? Mshirikishe mwenzio naye ajifunze zaidi.