Je! Unatakiwa kumwambia mwenza wako idadi ya uliofanya nao ngono?

0
36

Kumuuliza mpenzi wako kuhusu historia yake ya ngono inaweza kuwa kama kutazama filamu ya kutisha, unataka kujua kinachoendelea lakini pia hutaki kujua. Wataalamu wa mahusiano wanaeleza kuwa kufanya hivi kunaweza kuwa na faida lakini pia hasara kwa upande mwingine.

Hizi ni faida na hasara za kuweka wazi idadi ya wapenzi wako wa zamani ulioshiriki nao ngono.

Sio lazima kuweka siri
Sarah Ryan, mtaalam wa mahusiano anaamini kuwa muwazi kunaweza kusaidia kupeleka uhusiano wako katika kiwango kinachofuata, kwa kuwa uhusiano unaodumu hujengwa kwa mambo mawili ya msingi ikiwa ni uaminifu na heshima.

Kwanini wanaume, kwa wastani hufa kwanza?

“Ikiwa uko kwenye uhusiano ambao unataka yafike mbali, basi kwanini ujizuie kutoa uzoefu wako kutoka kwa wenza wako wa zamani? Kuzuia mambo kwenye maisha kunahitaji nguvu zaidi kuliko kukabiliana nayo na  kuyachilia,” anasema

Matukio yako ya zamani ni sehemu ya jinsi ulivyo leo.

Bila shaka uzoefu wako wa zamani wa kimapenzi na ngono huchangia kukuunda jinsi ulivyo, na jinsi unavyoishi katika mahusiano yako ya sasa, hivyo inaweza kumsaidia mwenza wako kukuelewa zaidi.

Je! Nini hasara ya kuwa muwazi juu ya idadi ya wapenzi ulioshiriki nao ngono?

Ukosefu wa usalama
Mtaalam wa uhusiano wa NYC na Mwandishi wa Breakup Triage, Susan Winter anasema kufafanua kwa kina kuhusu historia yako ya zamani ya ngono kunaweza kusababisha matatizo kwa mwenzi wako, kwa kuwa aina hii ya habari huleta ulinganisho na ukosefu wa usalama kwenye mahusiano.

Inaweza kuwa ishara kwamba mwenzi wako anadhibiti sana.

Ikiwa mpenzi wako anauliza juu ya hili kwa hali ya kawaida, basi hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, lakini ikiwa anakushinikiza au kukashifu, unapaswa kulitafakari hilo.

Ishara ya uhusiano mzuri ni kuhisi kama unaweza kumwambia mwenza wako ikiwa unataka, lakini sio kuhisi kama lazima ufanye hivyo. Ikiwa anakulazimisha kutaja idadi ya watu ulioshiriki nao mapenzi, inaweza kuwa dalili za kutaka kukudhibiti, inaweza kusababisha madhara zaidi kuliko manufaa.

Kulingana na Dk. Robi Ludwig, mtaalamu wa magonjwa ya akili anasema
watu wanataka kujua kuwa wako na mtu ambaye amekuwa na historia nzuri ya mapenzi huko nyuma, lakini maelezo ya maisha ya ngono ya mtu mara nyingi ni ngumu kwa mtu yeyote kuyafurahia kwani  inaweza kusababisha madhara kwenye uhusiano hasa mwanzoni.

Mwisho wa siku namba ni namba, hivyo hakikisha hujitesi sana kuhusu kujua uzoefu wake. Ikiwa mpenzi wako hataki kukuambia idadi ni sawa kuuliza kwa nini, lakini usimlazimishe kujua kwani unapaswa pia kuheshimu faragha yake.

Send this to a friend