Je Wajua? Bongo Zozo ni mbobezi kwenye kamari ya karata (poker)

0
44

Nick Reynolds (41) raia wa Uingereza ambaye ni maarufu zaidi nchini Tanzania kwa jina la Bongo Zozo ni mmoja ya wacheza kamari ya karata (poker) maarufu.

Katika taarifa ya mwaka 2018 ya mtandao maarufu wa mchezo huo duniani wa Poker News wasifu wa Bongo Zozo umeeleza kuwa hupenda kusafiri kwenda maeneo mbalimbali duniani kwa kucheza poker, na kwamba huwa anafurahia sana mchakato mzima anaopita wakati akiwa katika mashindano ya poker.

Kwa mujibu wa mtandao huo, baadhi ya maeneo ambayo Bongo Zozo amewahi kutembelea ni pamoja na Hispania, nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwamo Tanzania ambapo ndipo alijifunzia kucheza poker, na Slovenia. Mtandao huo haujaweka wazi sehemu gani hasa Tanzania amejifunzia mchezo huo.

2018 alishiriki mashindano ya mwaka ya Poker (WSOP) huko Las Vegas, Marekani.

“Mwaka jana (2017) nilipata fedha nyingi sana, badala ya kukaa na kufanya vitu vya kawaida ambavyo ni kuendelea kukusanya fedha hadi unazeeka na kuwa na mvi unashindwa kusafiri, niliwaza kuanza kuzunguka duniani na kucheza poker,” amesema.

Miongoni mwa mambo anayoyapendelea ni pamoja na kupanda milima ambapo hadi sasa amepanda Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania na Safu ya Milima ya Alps barani Ulaya.

“Napenda kujaribu vitu vipya, chakula kipya, watu wapya na kujifunza lugha mpya,” amesema.

Uchezaji wa poker sio njia pekee inayomuingizia kipato, bali pia amewekeza kwenye fedha za mtandao (cyptocurrency), biashara ya kuuza kahawa na kuuza fedha za Zimbabwe katika mtandao wa eBay.

Send this to a friend