
Mahakama ya Wilaya Singida imemhukumu Athumani Jumanne Mwangi (24), mkazi wa Mungumaji, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema mshtakiwa huyo alikamatwa akiwa na majani na misokoto 162 ya bangi yenye uzito wa kilo 1.6.
Hakimu Alocy Masua ametoa hukumu hiyo baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri.








