Jela miaka 30 kwa kumbaka mdogo wake ili awe tajiri

0
65

Mahakama mkoani Iringa imemkuta na hatia Frank Kigomba (31) mkazi wa Kijiji cha Kising’a na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela pamoja na fidia ya shilingi laki 5 kwa kosa la kumbaka mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 kutokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 2 mwaka huu saa 10 alfajiri ambapo alikwenda chumbani kwa mdogo wake na kumuita kwa nia ya kwenda kuingiza mbao kwenye nyumba aliyokuwa anajenga, ndipo akamkamata kwa nguvu kisha kumvua nguo na kumbaka.

Askari TANAPA auawa kwa mshale wenye sumu

Kamanda Bukumbi amesema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa mtuhumiwa alishauriwa kutenda kosa hilo na mganga wa kienyeji akidai kuwa akifanya mapenzi na mdogo wake atapata utajiri.

Mahakama ilimpandisha kizimbani Januari 5 ambapo mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuhukumiwa kwenda jela.

Send this to a friend