Jela miaka mitano ukimwanika mtoa taarifa za uhalifu

0
15

Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Amani Manyanga amebainisha kuwa mamlaka au mtu yeyote anayepokea taarifa za siri kutoka kwa mtoa taarifa au shahidi kuhusiana na uhalifu anapaswa kuzitunza taarifa hizo, kinyume na hivyo atakabiliwa na adhabu ya kifungo, faini au vyote kwa pamoja.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya sheria na kanuni za ulinzi kwa watoa taarifa na mashahidi mkoani Morogoro amefafanua kuwa mpokea taarifa anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni 15 au vyote kwa pamoja.

Aidha, amesema ikiwa mtoa taarifa atabainika kuwa taarifa ni za uongo anaweza kukabiliwa na kifungo si chini ya mwaka mmoja jela au faini ya shilingi milioni tatu, au adhabu zote mbili kwa pamoja.

Manyanga ametaja viongozi au mamlaka ambazo mtoa taarifa anaweza kupeleka taarifa ni pamoja na mwenyekiti wa mtaa au mtendaji, mbunge, diwani au kiongozi wa taasisi ya dini.

Ufaransa yafunga shule kutokana na kunguni

Ameongeza kuwa viongozi au mamlaka pia zinaweza kukabiliana na adhabu endapo hatua hazitachukuliwa kutokana na taarifa za siri zilizotolewa na kusababisha uhalifu kuendelea kutokana na kutodhibitiwa.

Kwa mujibu wa wakili huyo, madhumuni ya kutoa taarifa hizo za siri yatazingatiwa iwapo ni kwa maslahi ya umma, kutozingatiwa kwa sheria au kutaka kuvunjwa kwa sheria au kulinda afya pamoja na usalama wa watu.

Send this to a friend