Jela miezi 18 kwa kudai ametekwa, kumbe alikuwa kwa mpenzi wake

0
50

Mwanamke mmoja huko California, Sherri Papini (39), amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya kutoa taarifa za uongo kwa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI) akidai kutekwa nyara.

Inadaiwa mwanamke huyo alitoweka Novemba, 2016 na kuonekana wiki tatu baadaye barabarani akiwa amejeruhiwa, huku akidai alitekwa na wanawake wawili waliovalia vinyago wanaozungumza Kihispania, ambao walimfunga minyororo chumbani wakimshikia bunduki na kumtia alama kupitia chombo chenye joto.

Mashtaka hayo yalisababisha mamlaka kufanya msako wa kina kuwatafuta waliodhaniwa kuwa watekaji wa Kihispania ambao ulifanyika kwa miaka kadhaa bila mafanikio.

Mnamo 2020, FBI iligundua kuwa alikuwa akiishi kwenye nyumba ya mpenzi wake baada ya kuunganisha DNA kutoka kwenye nguo yake na mpenzi wake ambaye pia alikiri kuwa utekaji nyara huo ulikuwa uwongo, huku akijijeruhi kama sehemu ya mpango huo.

Mwanamke huyo pia ameamriwa kulipa takribani $310,000 (sawa na TZS milioni 722. 92) kama marejesho ya dola 30,000 (takribani TZS milioni 70) alizopewa na serikali kutoka kwenye fedha za fidia za waathirika.

Send this to a friend