Jenerali Jacob Mkunda ateuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi la Ulinzi ya Tanzania

0
90

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

Rais Samia pia amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Send this to a friend