Jenerali Mabeyo amuaga Rais Dkt. Hussein Mwinyi

0
10

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo.

Ameyasema hayo leo wakati akizunguumza na Jenerali Mabeyo ambaye amefika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais Mwinyi kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria.

Dk. Mwinyi amemuelezea Jenerali Mabeyo kwamba ni kiongozi ambaye alifanya kazi zake vyema katika Jeshi hilo, na alimpa ushirikiano mkubwa yeye na viongozi wenzake wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, hatua ambayo ilimuwezesha kufanya mabadiliko mengi ndani ya Jeshi hilo.

Aidha, amemtakia kila la kheri katika maisha yake ya kustaafu baada ya kulitumikia Jeshi hilo na kufanya mambo mengi yatakayoacha alama.

Jenerali Mabeyo ametoa pongezi na shukurani kwa Dk. Mwinyi kwa kutekeleza vema uongozi wake uliotukuka na kusema kuwa Jeshi litaendelea kumkumbuka Dk. Mwinyi kwa busara na hekima katika kuzishughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi ambalo hatimaye limepata mafanikio makubwa.

Send this to a friend