Jenerali Mabeyo: Ukinichanja damu yangu ni JWTZ

0
49

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amesema safari yake katika jeshi imemuimarisha kiutendaji na kumjengea misingi mizuri.

Ameyasema hayo leo Juni 28 jijini Dodoma ashiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa golfu na hoteli ya nyota tano.

“Siku zote nimekuwa nikiwaambia  kuwa mimi ninachokifahamu ni jeshi. Nimetoka shule moja kwa moja nimeingia jeshini, nimeendelea jeshini, kwa hiyo ninachokijua ni jeshi. Ukichanja damu yangu imeandikwa JWTZ,” amesema Jenerali Mabeyo.

Aidha, amewashukuru wananchi kwa kuwa watulivu katika kipindi ambacho Tanzania ilimpoteza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa madarakani na kueleza changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika kipindi chake jeshini.

“Wakati najiunga na jeshi nimetokea vitani. Niliingia vitani nikiwa kijana mdogo. Yapo mambo mbalimbali yaliyotokea, mafuriko, majanga mbalimbali, moto n.k mpaka nimefikia Ujenerali, na katika kipindi changu ndio Tanzania ina experince [inakabiliwa] kumpoteza Rais akiwa madarakani, ilikuwa ni changamoto kubwa,” ameeleza Jenerali Mabeyo.

Ameongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasifika kwa nidhamu pamoja na kutekeleza majukumu yake kwa umahiri mkubwa kwa kuwa linajua nini linatakiwa kufanya na kwa ajili ya nini.

Send this to a friend