Jeshi la Polisi kuchunguza vifo vya watoto mapacha Tegeta

0
60

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linafanya uchunguzi wa vifo vya kutatanisha vya watoto mapacha ambao walifariki baada ya kunyweshwa uji na mama yao katika eneo la Tegeta.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Jumanne Muliro amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, ikiwemo Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGCLA) na pindi uchunguzi utakapokamilika, maelezo zaidi kuhusu chanzo cha vifo yatatolewa kwa umma.

Taarifa ya vifo vya watoto hao ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii Oktoba 5, 2024, ikimuonesha mama wa mapacha waliofariki, Mwajuma Amani, akisimulia jinsi watoto wake walivyoonekana kuwa na afya nzuri hadi walipokunywa uji na kisha hali yao ikabadilika.

“Nilikuwa nimewapa uji vizuri, lakini nikawakuta wanashindwa kupumua, wakapoteza fahamu. Niko katika hali ya kuchanganyikiwa na sijui hasa kilichowapata mapacha wangu,” amesikika akisema mama huyo katika video ambayo ilisambaa sana katika mtandao wa YouTube.

Hata hivyo, Polisi katika kituo cha polisi cha Mabwepande Chini, wamekusanya sampuli za uji na unga uliotumika kupika uji, ili kubaini ikiwa walikunywa uji wenye sumu ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Send this to a friend