Jeshi la Polisi lakanusha madai ya CHADEMA

0
49

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema kuwa limesikitishwa juu ya taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika katika eneo la Nanenane mkoani Morogoro.

Taarifa hiyo iliyokuwa ikisema “Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro wamezuia msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika eneo la Nanenane wamezuia kupita barabara ya Morogoro kwa kile walichodai kuwa kuna kikao cha viongozi wa @tanpol Morena Hotel wakati huo magari mengine yakiendelea kutumia barabara hiyo.”

Jeshi hilo limesema Mnyika hakuzuiwa bali ulikuwa ni utekelezaji wa makubaliano na viongozi wa CHADEMA na hakuna aliyetamka kuwa kuna mkutano wa tanpol Hotel ya Morena siku hiyo kama sababu ya kuwazuia wasipite barabara kuu.

Jeshi la Polisi limewaomba Watanzania kupuuzia taarifa hiyo ambayo si sahihi kwakuwa ni viongozi waliokiuka makubaliano kati yao na Jeshi.

Send this to a friend