Jeshi la Polisi lamshikilia Mbowe kwa tuhuma za kukiuka taratibu za kampeni

0
26

Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa tuhuma za kukiuka utaratibu wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augustino Senga amethibitisha kumshikilia kiongozi huyo pamoja na watu wengine ambao idadi yao bado haijapatikana.

Kamanda Senga amesema baada ya Mbowe kupokelewa uwanja wa ndege alitaka kuweka mkutano hapohapo, jambo ambalo si sahihi kwa kuwa vyama vyote viliwasilisha maeneo ya mikutano yao.

Mbali na hayo, amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayeenda kinyume na taratibu hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Send this to a friend