Jeshi la Polisi lasema halina utani

0
59

Kufuatia taarifa zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha utani kati ya Jeshi la Polisi na raia, Jeshi la Polisi limesema Jeshi hilo si taasisi iliyoundwa kwa ajili ya kufanya utani bali kutekeleza majukumu hahususi ambayo ni kulinda maisha ya watu na mali zao.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Februari 18, 2023 imekanusha kauli hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema ‘msiogope kuwatania polisi’ na kudai haikutolewa na Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi si taasisi iliyoundwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kufanya utani bali kutekeleza majukumu mahususi ambayo ni kulinda maisha ya watu na mali zao, kulinda amani na utulivu, kusimamia utekelezaji wa sheria, kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata wahalifu na kupeleleza kesi,” limesema Jeshi.

Aidha, Jeshi hilo limewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu na siyo kufanya utani.

Send this to a friend