Jeshi la Polisi latoa tamko ushauri Kinana

0
62

Siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana kumshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura kuhusu kufanya tathmini juu ya idadi kubwa ya askari wa usalama barabarani ambao husababisha kero kwa wananchi njiani, Jeshi la Polisi limeanza kulifanyia kazi ombi hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime Jeshi la Polisi limeanza kuweka mikakati mizuri ya utekelezaji ambao pia umepokelewa kwa maoni mengi kutoka Kwa wananchi.

“Taasisi yeyote hasa inayohudumia jamii moja kwa moja kama Jeshi la Polisi, ili utendaji wake uweze kuboreshwa kila mara na uendane na matarajio ya wananchi na wadau wengine ni lazima kupokea ushauri, maoni na malalamiko na kuyafanyia kazi kwa wakati ili kuboresha utendaji wake na kuwaondolea kero wananchi,” amesema.

Kinana akerwa na utitiri wa trafiki barabarani

Adha, amesema Jeshi la Polisi lipo wazi kupokea maoni na ushauri kutoka kwa mtu yeyote mwenye lengo la kuboresha kitengo chochote au utendaji wa Jeshi la Polisi kwa ujumla ili wananchi wapate huduma bora pamoja na kuondoa malalamiko

Send this to a friend