Jeshi la polisi lawakamata waliosababisha mauaji Kataya, Mtwara

0
70

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa watu waliofanya mauaji na uhalifu mwingine katika Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara ni sehemu ya wale walioondolewa Kibiti mkoani Pwani.

Akifanya mahojiano na kituo kimoja che redio visiwani Zanzibar, IGP Sirro ameeleza kuwa baada ya kuwaondoa wahalifu hao mkoani Pwani walikimbilia nchini Msumbiji na kuungana na wenzao na sasa wanataka kurudi nyumbani.

“… wengine tulipambana nao wakaona wameshindwa wakakimbilia Msumbiji, kwa hiyo kule wameungana na wenzao wanajipanga kurudi…”

Aidha, amesema jeshi la polisi limejipanga vizuri kudhibiti wahalifu hao pindi watakapoingia nchini.

Kuhusu tukio hilo lililowaacha wengi na huzuni pamoja na hofu, Sirro amesema wahalifu 300 waliingia nchini kuwa wamewakamata baadhi ya waliofanya mauaji, na wanaendelea na msako kuweza kubaini mtandao mzima.

“Ukifanya uhalifu kwa Mtanzania ujue lazima italipa, damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi.”

Ameongeza kuwa wahalifu hao waliokimbilia Kaskazini mwa Msumbiji watashughulikiwa bila kujali watakapojificha iwe Kenya, Uganda, Burundi au kwingineko.

Mapema Mei mwaka huu Tanzania ilipeleka vikosi vya kwenye mpaka wake na Msumbiji baada ya kuibuka kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo kutoka Kaskazini mwa Msumbiji.

Send this to a friend