
Jeshi la Polisi limesema linafanya uchunguzi juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ametekwa usiku wa kuamkia leo.
Aidha, Polisi wamesema wanaendelea kumsubiria Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusu tuhuma anazozitoa kwenye mitandao ya kijamii.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa lilimtumia Polepole barua ya wito ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa lakini bado hajatekeleza maelekezo hayo.







