Jeshi la Polisi: Tumeona video za askari, tunafanya uchunguzi pamoja na kumpima
Jeshi la Polisi Zanzibar limesema linamchunguza askari anayetuhumiwa kujiuhusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga) na kwamba endapo ikithibitika kuna ukweli wa jambo hilo, atafikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi.
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamisi Hamad wakati akizungumza na Nipashe akibainisha kuwa ofisi yake ina mpango maalum wa kuwasaka askari wake wote wenye hulka na kujihusisha na matendo ya aina hiyo.
“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kadhia hiyo ikiwemo kufanyiwa kipimo askari huyo ili kujidhihirisha kama kweli anafanya kitendo hicho. Ingawa tumeona video katika mitandao ya kijamii lakini hatuwezi kusema moja kwa moja kama ni kweli au siyo kweli,” amesema.
Aina za mali zisizoweza kugawanywa pindi wanandoa wanapotengana
Aidha, Kamishna Hamad amesema askari anapojihusisha na mapenzi ya jinsia moja hukosa uaminifu na ukakamavu katika jukumu lake la msingi la kulinda raia na mali zake na kuongeza kuwa ni kinyume na tamaduni za nchi.
“Hatufai, na atashindwa kufanya kazi za polisi, na hata heshima kwa jamii haitokuwepo. Kama unamtuma askari polisi wa aina hii akamkamate mhalifu, akifika huko anaweza hata akaguswa (..) sasa heshima iko wapi kwa Jeshi la Polisi.
“Hata hivyo picha zinazosambaa hazioneshi kuwa amevaa sare za polisi au kufanya kitendo hicho kwenye kituo cha polisi, hivyo isitafsiriwe kuwa Jeshi la Polisi ndio limefanya,” ameeleza