Jezi za Simba zaanza kuuzwa baada ya kuvuja

0
15

Wakati mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakisubiria kwa hamu uzinduzi wa jezi za msimu mpya utakaofanyika Septemba 4, 2021, shauku hiyo huenda imepungua baada ya jezi hizo kuanza kusambaa mitandaoni, na sasa zitaanza kuuzwa leo.

Taarifa za kuvuja kwa jezi hizo zimethibitishwa na Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam na kukosoa vikali tabia hiyo.

Kamwaga amesema kuwa Tanzania ndio inaingia kwenye biashara ya jezi, hivyo utani wa jadi unapoingia na kufika hadi kwenye kuvujisha jezi, soka halitakuwa.

“Kuna timu kama Coastal Union wametoa jezi lakini hazikuvuja, imefika Simba jezi imevuja. Hii ni Tabia mbaya. Kwanini uvujishe jezi ya Timu? Tukianza ‘utani wa jadi’ wa kuvujishana jezi, Tunapokwenda itakuwa ni vita”.

Kutokana na kuvuja huko, klabu hiyo imezitangaza rasmi katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Aidha, Kamwaga amesema kuwa uzinduzi wake uko pale pale, na kwamba jezi hizo zitapatikana Tanzania nzima na ziko za kutosha.

Hizi ni picha za jezi hilo;