Jezi za Simba zakwama nchini Ethiopia

0
77

Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema jezi mpya za Simba zilizotarajiwa kufika nchini kutokea China, zimeshindwa kuwasili Tanzania kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kwa ndege za mizigo nchini Ethiopia.

Akizungumza kwenye mahojiano na Wasafi Redio, msemaji huyo amesema kuwa sherehe za mwaka mpya nchini China zilichangia kucheleweshwa kwa jezi hizo kutokana na usafiri kuwa wa shida.

“Kutokana na sherehe za mwaka mpya China usafirishaji mizigo ulikuwa wakusuasua ikabidi Vunjabei aende China kuhakikisha Jezi hazichelewi ila zikaja kukwama Ethiopia kwasababu ya ndege za mizigo kuchelewa,” ameeleza.

Aidha, amewaambia mashabiki wa Simba kuwa jezi hizo mpya zitawasili nchini hivi karibuni kabla ya mechi ya Simba dhidi ya Raja Casablanca.