Jibu hivi unapoulizwa udhaifu wako kwenye usaili (interview)

0
59

Ubora na udhaifu wa msailiwa ni miongoni mwa maswali yanayohitaji umakini mkubwa sana katika kuyajibu kwani ni jawabu moja wapo linalosaidia kuelewa tabia binafsi za mwombaji.

Kipengele kinachohitaji umakini zaidi ni kwenye kuelezea udhaifu ulionao, pamoja na kwamba kila binadamu ana udhaifu wake lakini ni wachache sana wenye ujasiri wa kukubali mapungufu hayo na kuwa tayari kujirekebisha.

Msailiwa anaweza kuainisha udhaifu au upungufu alionao katika eneo la utendaji ambao hauna athari kubwa kwenye utekelezaji wa majukumu na kuonesha juhudi alizoshafanya kutatua upungufu huo.

Makosa 6 ya kuepuka unapoamka asubuhi

Mfano, unaweza kueleza udhaifu katika kupokea kwa haraka mabadiliko ya kiteknolojia na uhitaji wa muda kidogo ili kuelewa mabadiliko hayo kabla ya kuanza kuyatekeleza katika eneo la kazi.

Mfano wa udhaifu huu hauna athari ya moja kwa moja kwenye utendaji, zaidi unaweza kutafsiriwa kama umakini wa msailiwa katika kuchunguza kwa kina mambo kabla ya kuyajumuisha katika utaratibu wako wa kazi.

Kuhusu ubora wa kikazi, msailiwa anaweza kujibu katika kufafanua kuhusu ujuzi, taaluma, uzoefu wa utendaji na mchango katika kuleta matokeo chanya kwa kampuni au taasisi unayotarajia kufanya nayo kazi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend