Jiji la Mwanza lajitenga na Mgambo walioharibu bidhaa za Machinga

0
51

Halmashauri ya Jiji la Mwanza imewasimamisha kazi Askari Mgambo walionaswa kwenye mkanda wa video wakichukua ndizi mbivu za mjasiriamali na kuzitupa ndani ya gari la halmashauri, kisha kuondoka nazo.

“Halmashauri ya Jiji la Mwanza haihusiki kwa namna moja au nyingine kuagiza Askari Mgambo kuendesha zoezi hili kwa namna inavyoonekana, bali ni utashi na nia ovu ya askari hao,” imeeleza sehemu ya taarifa ya Mkurugenzi wa Jiji, Sekiete Yahaya.

Mbali na kusimamishwa kutojihusisha na operesheni ya kuwaondoa Machinga katika maeneo yasiyo rasmi, taratibu nyingine za kisheria zinaendelea kufanyika dhidi ya wahusika.

Halmashauri imewaomba radhi Wajasiriamali na Watanzania waliokumbana na kadhi hiyo na kusisistiza kwamba halmashauri inaongozwa kwa sheria, miongozo na taratibu, na kwa kuzingatia utu na maadili.

Send this to a friend