Jinsi ndege wanavyoweza kupunguza msongo wa mawazo

0
40

Ikiwa unataka kuboresha afya yako ya akili basi labda unapaswa kuanza kutenga muda kidogo kila siku kukaa na kusikiliza ndege wakilia nje ya madirisha yako.

Sayansi imeonyesha kuwa nyimbo ambazo ndege huimba zinaweza kuwa na matokeo ya kushangaza kwenye ubongo wako.

Je, ndege wanaweza kusaidia kwenye maisha ya kila siku?

Zaidi ya tathmini 26,000 zilizokusanywa na watafiti kati ya Aprili 2018 na Oktoba 2021, zimeonesha mwelekeo muhimu kuhusu jinsi ndege wanavyoweza kumsaidia mtu katika kuboresha ustawi wa akili kila siku. Watafiti wanasema kusikiliza sauti za ndege kila siku kunadumisha ustawi wa akili.

Kupunguza Mfadhaiko
Kwa mujibu wa watafiti wanasema sauti za ndege zinaweza kuwa tiba pia kwa mtu anayepitia sonona (depression), ugonjwa wa akili unaosumbua ulimwengu wote. Watafiti waligundua kwamba si tu kukutana na ndege na kusikiliza nyimbo zao kunasaidia afya ya akili, bali pia matokeo hayo yanadumu kwa muda mrefu baada ya kukutana na wanyama hao.

Mtaalamu: Wanawake wanachangia ongezeko la tatizo la nguvu za kiume

Nyimbo za ndege zinaweza kusaidia kupitia ‘earphones’
Mtafiti Emme Strobbe anaeleza kwamba jambo la pekee kuhusu nyimbo za ndege hata watu wanaoishi katika mazingira ya mijini ambako kusikia sauti za ndege ni nadra, wanaweza kutumia vifaa vya sauti kama earphone’ na ‘headphone’ kusikiliza sauti za ndege ambayo zitahusisha mazingira asilia.

Utafiti wa pili ulionyesha kwamba kusikiliza kipande cha sauti cha nyimbo za ndege kwa dakika sita tu kunatosha kupunguza hisia za wasiwasi, mfadhaiko, na hata wazimu.

Ikiwa mtu anafanya kazi au anatumia akili nyingi katika kufikiri ni vizuri kusikiliza sauti za ndege wakiimba ili kutuliza akili yako na kuiboresha katika ufikiri.

Send this to a friend