Jinsi ya kukabiliana na mke mwenye hasira na kisirani

0
62

Kuna sababu nyingi zinazosababisha mtu akajawa na hasira na kisirani. Washauri wa mambo wanasema usirudishe hasira kwa hasira badala yake dhibiti hisia zako. Hasira inaweza kuharibu uhusiano wako na hata kuvunjika kabisa kwa sababu tu ya kushindwa kuwa mtulivu na mvumilivu.

Haya ni mambo yatakayokusaidia kukabiliana na mke mwenye hasira na kisirani.

• Fanya vitu vitakavyoondoa hasira yake

Fanya vitu vya kawaida vinavyomtia wazimu na kurudisha tena furaha yake. Inakupasa uelewe sehemu au vitu hivyo na ikibidi zikariri kama vile wimbo wa taifa ikiwa kama utafanya kosa au jambo ambalo litaamsha hasira yake.

• Usitoe Sababu yoyote juu ya matendo yako

Wataalam waeleza sababu kuu 3 za wanaume kukosa nguvu za kiume

Anapojawa na hasira hakuna uwezekano wa kusikia upande wako wa hadithi, baki tu ukimtazama. Inapaswa kuonekana kuwa unazingatia kile anachosema. Kutofanya hivyo kunaweza kumkasirisha zaidi.

• Usibishane au kujaribu kuwasilisha madai ya kupinga.

Usijaribu kubishana naye na wala usimwombe atulie, Haya ndiyo aina ya mambo ambayo yanaongeza nguvu zaidi kwenye hoja na yatakayomfanya aendelee kuongea zaidi. Ni bora kukaa kimya.

• Jisalimishe Kwake

Tumia lugha ya mwili wako kuonyesha kwamba unakubaliana na sababu yake ya kukasirika. Kwa mfano, tikisa kichwa chako mara kwa mara anapozungumza. Kutofanya hivyo kutamfanya apige kelele zaidi.

• Usimkimbie

Kwa wanawake wengi, hasira ya maneno husababishwa na masuala ya homoni ambayo hayaepukiki. Kwa hivyo, unaweza kumsaidia na kuhakikisha kuwa siku si nyingi kutakuwa na amani. Kutoroka eneo la tukio itamfanya achukie na kufadhaika zaidi. Zaidi ya hayo huwezi kumuepuka kila siku.

• Omba msamaha

Mara nyingi, hasira huongezeka kutokana na masuala ya kina. Pengine anakasirishwa kutokana na matendo yako, hivyo jitafakari kisha umuombe msahama na kujirekebisha.

• Mtafutie mshauri

Ikitokea kwamba kuna masuala mazito ya kihisia yanayomlemea mke wako, jaribu kuzungumza naye au mwambie kwamba utaongozana naye kwa mshauri. Mke wako anahitaji utegemezi wako ili kuruhusu mambo yaliyopita yapite na kujisamehe mwenyewe au mtu mwingine ambaye alimuumiza wakati uliopita.