Jinsi ya kuondoa taarifa zako binafsi Google

0
25

Ikiwa kuna habari kwenye Google ambayo unahisi ni nyeti na inaweza kuleta athari kwako mwenyewe na watu wako wa karibu, kuna njia ya kuiondoa kwenye mtandao.

Huduma ya Tafuta na Google ina sera zinazowaruhusu watumiaji kuomba kuondolewa kwa maudhui fulani kwenye huduma ya Tafuta na Google, kwa kulenga maudhui binafsi ambayo yakiwa hadharani yanaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja kwa watu.

Hivi ndivyo jinsi ya kuondoa taarifa binafsi kwenye google:

1. Nenda kwenye jukwaa la usaidizi la google (Google Help) kwenye: https://support.google.com/
2. Kisha nenda ‘kuondoa taarifa zako binafsi kwenye Google ‘(‘to remove your personal information on Google’)
3. Chagua ‘Omba kuondoa maelezo yako binafsi kwenye Google’ (‘Request to remove your personal information on Google’)
4. Jaza fomu ya mtandaoni ili kuwasilisha ombi la kuondolewa.

Kulingana na Google, maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu (PII), unayoweza kuomba yaondolewa kwenye google ni pamoja na:

 Namba za siri za utambulisho wa serikali (ID).
 Namba za akaunti ya benki
 Namba za kadi ya mkopo
 Picha za saini zilizoandikwa kwa mkono
 Picha za hati za kitambulisho
 Rekodi za kibinafsi, zilizowekewa vikwazo na rasmi, kama vile rekodi za matibabu
 Maelezo ya mawasiliano ya kibinafsi (anwani za mahali, nambari za simu, na barua pepe)

Kumbuka: Google inaweza isiondoe taarifa yako binafsi kwenye matokeo yake ya utafutaji ikiwa taarifa hiyo imejumuishwa kwenye habari. Mfano, ikiwa inaonekana katika makala ya habari husika au ikiwa imejumuishwa kwenye tovuti ya serikali au chanzo kingine rasmi.

Send this to a friend