JKCI kuja na tiba ya upungufu wa nguvu za kiume

0
41

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuanza kutoa tiba ya kuzibua mishipa ya uume ili kukabiliana na upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wanaokabiliwa na shida hiyo.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge amesema taasisi hiyo imefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza mdogo wa moyo kwa kuzibua mishipa ya damu ya miguuni iliyoziba, na huduma hiyo kwa wanaume wenye changamoto ya nguvu za kiume inatarajiwa kuanza kutolewa Oktoba mwaka huu.

Kinywaji cha ‘kuongeza’ nguvu za kiume chapigwa marufuku

“Oktoba tutaanza kutoa huduma mpya tukishirikiana na wenzetu wa India, tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni kubwa na linazidi kuongezeka kutokana na mishipa ya uume kuziba, na hivyo mwanaume anashindwa kuhimili,” amesema.

Ameongeza kuwa tatizo hilo ni kubwa japo hakuna utafiti walioufanya, na kwamba wapo wanaume wenye tatizo hilo wanaofika JKCI wakihitaji huduma.

Send this to a friend