JPM: Sikutengeneza barabara za Kibamba kwa sababu sikuombwa

0
36

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa hakutengeneza barabara za Jimbo la Kibamba mkoani Dar es Salaam kwa sababu hakuombwa kufanya hivyo, na kufafanua kuwa, kunapokesakana muunganiko wa viongozi, ni vigumu maendeleo kupatikana.

Dkt. Magufuli amesema hayo wakati akizindua stendi ya mabasi ya kimataifa iliyopo Mbezi Luis ambapo amesema inashangaza na kushtua kusikia kwamba jimbo hilo lina kilomita 5 tu barabara zenye lami.

Amesema kuwa hali hiyo inashangaza sana na ni vigumu mtu kuamini kama eneo hilo lilikuwa na viongozi.

Akihutubia wananchi katika hafla hiyo, amemuagiza Waziri wa Ujenzi na mamlaka nyingine zinazohusika kuangalia barabara za jimbo hilo na Ubungo kuona ni barabara zipi zianze kujengwa.

Ametumia jukwaa hilo kumpongeza Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu ambaye katika salamu zake alieleza hali ya barabara jimboni humo na kumuomba Rais Dkt. Magufuli kujenga kama alivyoahidi wakati wa kampeni.

Send this to a friend