Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda ameamuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kushiriki operesheni ya kuzima moto unaoendelea kusambaa ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Maafisa na Askari wa JWTZ tayari wamewasili maeneo ya Siha na Mwika Mkoani Kilimanjaro tayari kuanza operesheni ya uzimaji wa moto huo.
JWTZ imesema itashirikiana kikamilifu na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, wadau mbalimbali na wananchi ili kuhakikisha moto huo unadhibitiwa mapema kabla ya kuleta madhara makubwa katika hifadhi hiyo.