JWTZ: Tunaingia mtaani kuzisaka sare zetu kwa wananchi

0
60

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.

Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.

“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.

Nay wa Mitego ashitakiwa kwa uchochezi

Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.

Chanzo: Habari Leo

Send this to a friend