JWTZ yamsaka aliyesambaza uzushi mitandaoni
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taaria zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamiii kupitia ukurasa wa X (iliyofahamika kama Twitter) wa Tanzania Abroad TV kwamba wanajeshi wa ngazi za juu wa JWTZ wameongezewa mshahara.
JWTZ imesema taarifa hiyo iliyodai kuwa ongezeko hilo limelipwa Agosti 18, 2023 ni ya uzushi na yenye lengo la upotoshaji kwa jamii, hivyo kuwataka Watanzania waipuuze.
“Ukweli ni kwamba hadi leo Agosti 19, 2023 kwa JWTZ haijafika tarehe ya kulipwa mshahara. Hakuna ongezeko lolote la mishahara au malipo yoyote kwa wanajeshi wa ngazo yoyote wa JWTZ yaliyofanyika Agosti 18, 2023 kama ilivyotajwa na mtandao huo,” amesema.
Wawekezaji 10 wanaoongoza kwa mtaji mkubwa Soko la Hisa la Dar es Salaam
Aidha, JWTZ limesema linaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji huo ili hatua za kisheria zifuatwe.